Yanga SC

DUH..KUMBE HII NDIO SABABU YA YANGA KUKATAA MECHI NA TIMU ZA MOROCCO

admin August 29, 2021 5:30 am


WACHEZAJI wa Yanga wameenda moja kwa moja kambini kuungana na wenzao waliorejea siku chache zilizopita.

Yanga nao waliweka kambi nchini Morocco ikiwa ni maandalizi ya michuano mbalimbali ambayo itakutana nayo msimu ujao.

 Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema, wachezaji wao wanaelekea kambini moja kwa moja kuungana na waliotangulia.

Anasema walitamani kuwapa mapumziko mafupi wachezaji wao Baada ya kurejea Ila kutokana na ratiba kuwabana wameona ni vyema  waende kambini kuungana na wenzao.

“Ingekuwa ngumu kuwaruhusu kwenda nyumbani kutokana na tukio la kesho la wiki ya wananchi,”

“Tukio la kesho {leo} ni muhimu Sana hivyo wachezaji wetu kuwepo ni muhimu japokuwa kuna wengine walioko kwenye timu za Taifa watakosekana, “

Aidha Mwakalebela amesema ratiba ilibana na ndio sababu kubwa iliyopelekea kukosa mchezo wa kirafiki walipokuwa kwenye kambi yao Morocco ambayo ilivunjwa kwasababu mbalimbali ikiwemo hali ya hewa.

Amesema Baada ya hitimisho la kilele cha Mwananchi kesho{leo} wataendelea na maandalizi na timu itapata mechi nyingi za kirafiki.

VIDEO: TAZAMA NAMNA WACHEZAJI YANGA WALIVYOPOKELEWA BAADA YA KUHAMIA YANGA…MANARA ATOA MSHAHARA WAKE WOTE KWA MATHIAS MDAMU..AMTAJA GSM

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply