Home news BAADA YA KUMALIZANA NA TAMBWE..TIMU TAJIRI DARAJA LA KWANZA WASHUSHA MASTAA HAWA...

BAADA YA KUMALIZANA NA TAMBWE..TIMU TAJIRI DARAJA LA KWANZA WASHUSHA MASTAA HAWA WENGINE


Klabu ya DTB (Diamond Trust Bank) FC itakayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, imekamilisha usajili wa Mshambuliaji kutoka Burundi Amisi Tambwe.

Tambwe amerejea Tanzania akitokea Djibout alipokua akiitumikia Klabu ya Polisi inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Kabla wa kuondoka nchini Amisi Tambwe aliwahi kuvitumikia vilabu vya Simba SC na Young Africans kwa nyakati tofauti.

Mbali na usajili wa Tambwe pia klabu DTB FC imekamilisha usajili wa Tafadzwa Kutinyu raia wa Zimbabwe ambaye aliwahi kuitumikia Singida United, Azam FC na AC Horoya ya Guinea.

Aidha DTB FC imekamilisha usajili wa Juma Abdul Mnyamani nyota wa zamani wa Young Africans na Owen Chaima raia wa Malawi ambaye aliwahi kuitumikia Mbeya City na Singida United.

SOMA NA HII  UCHAGUZI MKUU SIMBA: MANGUNGU ABADILI UPEPO ...KALUWA APIGIWA YOWE UKUMBI MZIMA...