Home Yanga SC HAJI MANARA:SISI TAMASHA LETU LILIDODA MWAKA JANA, YANGA WALITUZIDI

HAJI MANARA:SISI TAMASHA LETU LILIDODA MWAKA JANA, YANGA WALITUZIDI


 KUELEKEA kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, Agosti 29, Haji Manara ameweka wazi watafunika zaidi ya ile ya mwaka 2020 na ameweka wazi kwamba wao tamasaha lao lilibuma mwaka jana.

Manara ameibuka ndani ya Yanga akitokea Simba ambapo aliweza kuhamasisha mashabiki wa timu hiyo kuweza kujitokeza kwa wingi katika tamasha la Simba Day ila kwa wakati huu anahamasisha watu wajitokeze Mwananchi Day.

Tamasha hilo kwa sasa linaendelea ambapo mashabiki Tanzania wamekuwa wakiendelea kutoa misaada kwa jamii na kutoa damu pamoja na kufanya usafi huku kilele kikitarajiwa kuwa Agosti 29, Uwanja wa Mkapa na utapigwa mchezo wa kirafiki.


Manara amesema:”Sisi tamasha letu lilidoda mwaka jana tulipigwa bao na Yanga ila kwa ubishi wangu na kujitutumia ikaonekana kama tuko sawa, sasa kwa sasa nikiwa nimekuja huku unadhani nini kitatokea?

“Yanga wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa jambo ambalo limenifanya nije huku sasa. Tulifunga screen pale uwanja wa jirani ila zilidoda waliingia watu 20 tu tofauti na wenzetu,” .

SOMA NA HII  KUHUSU YANGA KUSAJILI KIFAA CHA REAL BAMAKO...UKWELI UKO HIVI...MORRISON MGUU NDANI MGUU NNJE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here