Azam FC

LWANDAMINA: TUNAREJESHA UTIMAMU WA WACHEZAJI

admin August 26, 2021 7:43 am


GEORGE Lwandamina,  Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wake walikuwa wanafanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika mchezo wa kirafiki dhidi Red Arrows. 

Kwenye mchezo huo wa kurejesha utimamu wa mwili Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 huku Lwandamina akiweka wazi kuwa kuna jambo ameliona kwa wachezaji wake.

“Nilikuwa nataka kuona wachezaji wanarejea katika utimamu wa mwili hasa kutokana na uchovu pamoja na kukaa muda mrefu bila kucheza mechi za ushindani.

“Hata namna wachezaji walicheza bado walionekana hawajawa tayari hivyo taratibu wanarejea katika hali ya kawaida ni jambo la kusubiri,” amesema. 

Azam FC imeweka kambi nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22 na itawakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ikiwa ipo kwenye Kombe la Shirikisho.

NDEMLA NDIO BASI TENA MSIMBAZI…ARUDISHWA BONGO KIMYA KIMYA…KUVAA UZI WA KIJANI AU… SAKATA LA MORRISON NA YANGA NGOMA BADO MBICHI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply