Home Simba SC SIMBA WAREJEA TANZANIA SALAMA

SIMBA WAREJEA TANZANIA SALAMA


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo kimewasili Tanzania kikitokea nchini Morocco.

Timu hiyo iliweka kambi nchini Morocco na safari ilianza jana kupitia Dubai ambapo kilikuwa huko.

Simba baada ya kumaliza kambi wanatarajiwa pia kuweka kambi nyingine baada ya ile ya awali kukamilika.

Wanachosubiri kwa sasa ni kuungana na wachezaji waliopo timu ya taifa ili waendelee na maandalizi ya msimu wa 2021/22.

Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kambi ilikuwa salama na wanaamini msimu ujao kila kitu kitakwenda sawa.

Wamerejea na wachezaji ambao walijiunga na Simba katika dirisha kubwa ikiwa ni pamoja na Peter Banda.

SOMA NA HII  ISHU YA OUATTARA NA SIMBA YAZIDI KUPASUA KICHWA...BOSI AFUNGUKA NAMNA JAMBO LILIVYO NDANI KWA NDANI...