Home Simba SC SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA LUIS KUIBUKIA YANGA, KUTAMBULISHWA SIKU YA MWANANCHI

SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA LUIS KUIBUKIA YANGA, KUTAMBULISHWA SIKU YA MWANANCHI


 BAADA ya tetesi kueleza kuwa kiungo aliyekuwa mali ya Simba msimu wa 2020/21 Luis Miquissone kwamba ataibukia kwa watani zao wa jadi Yanga, uongozi wa timu ya Simba umesema kuwa suala hilo halipo kwa wakati huu.

Luis msimu ujao wa 2021/22 hatakuwa mali ya Simba baada ya uongozi wa timu hiyo kubainisha kwamba hatakuwa ndani ya kikosi hicho kwa wakati ujao na hawajaweka wazi timu ambayo atakuwepo msimu ujao.

Habari zinaeleza kuwa Luis atakuwa ni mali ya Al Ahly ya Misri na uvumi ukaeleza kwamba atatambulishwa Yanga siku ya Mwananchi, Agosti 29, Uwanja wa Mkapa.

Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wengi wanasema mambo ambayo hayapo na hivyo hakuna jambo hilo.

“Wengi wanasema kwamba kwa sasa Luis atakwenda Yanga, jambo hilo sio kweli kwani mchezaji huyo amepata timu nje na sio huko anakotajwa kwenda,” .

SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO DABI KESHO...HUU HAPA UTAMU AMBAO HUPASWI KUUKOSA ...