Home Yanga SC YANGA WAFUNGUKA SABABU ZA MAKOCHA WAO KUTOWEKA

YANGA WAFUNGUKA SABABU ZA MAKOCHA WAO KUTOWEKA


UONGOZI wa klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa upo katika mazungumzo ya kuwaongeza mikataba kocha msaidi wa timu hiyo, kocha wa viungo na daktari wa misuli mara baada ya mikataba yao ya awali kutamatika ndani ya Yanga.

Kocha Msaidizi, Sghir Hammadi mwenye uraia wa Tunisia, kocha wa viungo Mmorocco, Jawab Sabri na Mchua misuli wa Yanga  mwenye uraia wa Afrika Kusini, Fareed Cassiem wote hawapo katika kambi ya Yanga iliyopo nchini Morocco.

Yanga kwa sasa ipo nchini Morocco ambapo klabu hiyo imeweka kambi maalumu ya siku 10 kwa ajili ya  maandalizi ya msimu mpya, wa michuano mbalimbali ambayo Yanga itashiriki katika msimu ujao.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimetuambia kuwa makocha hao wote watatu wamemaliza mikataba yao, huku wengine wakiwa wapo katika mazungumzo na timu nyingine japo klabu ya Yanga wapo katika mazungumzo ya kuwaongezea mikataba mipya.

β€œNi kweli makocha hao wote mikataba yao imetamatika ndani ya Yanga, na wapo ambao walikuwa kwenye mazungumzo ya kujiunga na klabu zingine huku Yanga nao wakifanya nao mazungumzo ya kuhitaji kuwaongezea mikataba mipya.

Akizungumzia sakata hilo Ofisa habari wa Yanga Hassani Bumbuli amesema: β€œMikataba ya makocha hao imemalizika hivyo kama klabu tupo katika mipango ya kuwaongezea mikataba mipya hivyo wanaweza wakaonekana msimu ujao, au wasionekane,” Amesema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  WAKATI FEI TOTO AKIONEKANA DUBAI....YANGA SC WAIBUKA NA KUTOA MSIMAMO HUU...