Home Cecafa Cup YANGA YAFUNGASHIWA VIRAGO KAGAME CUP, UWANJA WA MKAPA

YANGA YAFUNGASHIWA VIRAGO KAGAME CUP, UWANJA WA MKAPA


 KIKOSI cha Yanga leo kimefungashiwa virago kwenye mashindano ya Kagame Cup 2021 baada ya kupoteza mbele ya Express FC.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-3 Express FC ambapo ni mabao ya Godfrey dk 14, Muzamiru dk 35 na Kambale dk 52 walipachika mabao kwa Express.

Bao pekee la Yanga limefungwa na Paul Godfrey dk 71 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 ambalo liliamsha nguvu kwa Wananchi lakini walishindwa kupata ushindi.

Inakuwa ipo nafasi ya tatu na pointi mbili kwenye msimamo huku Express wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 7.

Timu nyingine kutoka kundi A ambayo imetinga hatua ya nusu fainali ni Big Bullets ya Malawi ambayo ina pointi 5 kibindoni.

SOMA NA HII  YANGA YAFANYA USAJILI HUU...MAYELE AFICHUA SIRI JANGWANI...BOCCO AMVUTA KIUNGO HUYYU MPYA SIMBA