news

RASMI..MAGORI AVAA VIATU VYA MANARA SIMBA..ATUPA DONGO JANGWANI

admin September 1, 2021 6:00 pm


Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzj Simba SC, Crescentius Magori ameibeza klabu ya Young Africans kwa kusema kikosi chao kilicheza na Vibonde Siku ya Mwananchi.

Magori amesema amesema Zanaco FC iliyoifunga Young Africans siku ya Jumapili (Agosti 29) ni timu ya kawaida sana.

Amesema Young Africans haikupaswa kupoteza mchezo kwa kufungwa 2-1 na Zanaco FC ambayo haipo kwenye orodha ya vilabu 10 bora Afrika.

Maagori amewataka wadau wa Soka nchini kujiandaa kuona burudani safi katika Tamasha la SIMBA DAY itakapofika Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.

“Jumapili nimeangalia mpira mpaka nimesinzia, Wanacheza mpira gani ule wanacheza kama wanatembea Pressing yao ni ndogo sana.”

“Tarehe 19 ndiyo mtaona mpira sasa, yaani utapigwa mwingi watu wataangikana aaaaaaah.”

“Wamecheza na Zanaco ambayo haipo hata kwenye list ya vilabu 10 bora Afrika na wakapigiwa mpira mwingi vile, waje tarehe 19 wamuone Rally Bwalya, Pape Sakho na mafundi wengine ndo wajue Mpira unavyochezwa.”

Hata hivyo Simba SC bado hawajatangaza timu itakayocheza dhidi ya kikosi chao katika Tamasha la Simba Day, Septemba 19.

Kwa madongo hayo kwenda Yanga ni dhahiri shari sasa Wekendu wa msimbazi Simba, hawatakuwa na haja na msemaji wa kutoa maneno ya ‘kukera’ kwani Magori anaonekana kuiweza kazi hio.

MUBEEN ESMAIL ASHINDA JACPOT YA SportPesa TWAHA KIDUKU: MWAKINYO ANAJIBIWA ULINGONI, WATU WANATAKA SHOW

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply