news

KIM POULSEN MATUMAINI KIBAO MBELE YA MADAGASCAR

admin September 3, 2021 6:44 am


KIM Poulsen,  Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa mchezo wao wa jana dhidi ya DR Congo ulikuwa ni mgumu ila anawapa pongezi wachezaji wake kwa kupambana.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa TP Mazembe,Lubumbashi ngoma ilikuwa ni 1-1 na kuwafanya wagawane pointi mojamoja. 

Kim amesema:”Mchezo wetu ulikuwa mgumu hasa kutokana na wapinzani wetu ambao walikuwa bora na kuweza kumiliki mpira kwa muda kipindi cha kwanza na kupata bao ambalo tuliweza kusawazisha.

“Kwa namna wachezaji walivyopambana wanastahili pongezi kwa kuwa wamefanya kazi kubwa dhidi ya mpinzani wetu ambaye alikuwa imara.

“Makosa yapo na tuliyafanyia kazi kipindi cha pili kuelekea katika mchezo wetu ujao dhidi ya Madagascar tutapambana kupata ushindi na tunaamini kwamba tutapata ushirikiano kutoka kwa mashabiki, ” amesema.

Mchezo ujao wa Tanzania unatarajiwa kuchezwa Septemba 7, Uwanja wa Mkapa.

MANCHESTER UNITED KUTUMIA MBINU HII KUINASA SAINI YA HAALAND SAUTI:YANGA YAIFUNIKA SIMBA ISHU YA USAJILI, YAMWAGA MKWANJA MREFU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply