news

UZI MPYA WA SIMBA 2021/22 HUU HAPA

admin September 3, 2021 10:43 am


 KLABU ya Simba imeweka wazi kuwa kwa sasa jezi mpya kwa msimu wa 2021/22 zinapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei.

Ezekiel Kwamwaga, Kaimu Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa Simba kuzihitaji jezi hizo wakaona hakuna tatizo wakaamua kuziruhusu zipatikane madukani.

“Awali ilikuwa tumepanga kuzindua rasmi Septemba 4 kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa Simba tumeamua kuziruhusu kupatikana katika maduka ya Vunja Bei.


“Ni jezi nzuri na bora na kila shabiki ajivunie na apate jezi yake orijino nina amini kwamba hakuna ambaye ataweza kupenda kuona anavaa kitu feki hilo halipo hivyo kila mmoja ajipatie jezi mpya.

“Kuhusu uzinduzi siku ya Jumamosi bado upo palepale na tutatoa utaratibu namna mambo yatakavyokuwa ni suala la kusubiri na kuona,” .

SIMBA YAJA NA SLOGAN MPYA,VIINGILIO VYATAJWA KUELEKEA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA NA SHIRIKISHO..CAF WASHUSHA RUNGU TZ..WAFUNGIA UWANJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply