news

HAJI MANARA: YANGA INA MATAJI MENGI KULIKO TIMU YOYOTE

admin September 10, 2021 4:43 am


 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa timu yenye makombe mengi ndani ya Tanzania ni Yanga na hao ni mabingwa wa muda wote.

Awali alipokuwa ndani ya Simba kabla ya kubwaga manyanga aliwahi kuweka wazi kuwa timu hiyo ya Simba ilikuwa ni namba moja kwa kutwaa mataji mengi ila kwa wakati huu anasema kuwa Yanga ni mabingwa mara nyingi.

Manara ameweka wazi kuwa huwezi kusema kuwa Simba amechukua Kombe ubingwa mara sita wakati Yanga amechukua mara tano wakati kuna data nyingine ambazo hazijawekwa.

“Mabingwa wa muda wote ndani ya Tanzania ni Yanga, hizo namba zote ambazo unaziona nilizitengeneza mwenyewe, hivyo haziwezi kunitisha kabla ya kujiondoa.

“Ikiwa utaweka orodha ya mabonanza pamoja na mambo mengine basi Yanga inaweza kuwa na mataji bilioni ambayo tumeyatwaa hivyo hakuna namna kwa fact, (ukweli) sisi tunaongoza kwa kutwaa mataji mengi.

“Achana na porojo za nyuma kwa fact Yanga ina mataji mengi kuliko klabu yote Tanzania, nilifanya makosa ya kudangaya,” .  

MECHI ZOTE ZA AZAM FC KIMATAIFA KUPIGWA DAR WANAJESHI WA MPAKANI, KAZINI LEO KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply