Home Azam FC MECHI ZOTE ZA AZAM FC KIMATAIFA KUPIGWA DAR

MECHI ZOTE ZA AZAM FC KIMATAIFA KUPIGWA DAR


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Horseed FC unaotarajiwa kuchezwa kesho, Septemba 11, Uwanja wa Azam Complex.

Pia mechi zote mbili zitachezwa Dar ikiwa ni ile ya kwanza ambapo Azam FC watakuwa ni wenyeji na ile ya pili ambayo Horseed ya Somalia watakuwa wenyeji.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo muhimu.

Pia ameongeza kuwa kwa maelekezo ya Shirikisho la Soka Afrika, CAF, mchezo huo wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, utakaochezwa kesho Jumamosi saa 1.00 usiku, hautokuwa na mashabiki.


“Maandalizi yapo vizuri na kwa taarifa kutoka kwenye benchi la ufundi ni kwamba wachezaji wamekuwa wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya kuwa tayari na mchezo wetu dhidi ya wapinzani wetu.

“Mashabiki wetu bado tupo nao bega kwa bega hivyo dua zenu ni muhimu. Kikubwa ni kuweza kufuatilia mchezo kupitia Azam TV pamoja na radio U FM zote zitakuwa mubashara.

“Hata mchezo wa pili nao utachezwa Dar Uwanja wa Uhuru, hivyo tutapambana kupata matokeo chanya,”.

Kwa sasa kikosi kinaendelea na mazoezi Dar baada ya kuweka kambi ya muda nchini Zambia, Ndola ambapo kilicheza michezo ya kirafiki kujiweka sawa.
SOMA NA HII  IKIWA IMEPITA MIEZI KADHAA TOKA ASEPE ....HITIMANA KAONA ISIWE TABU...KAFUNGUKA HAYA KWA SIMBA...