news

MECHI ZA KIMATAIFA KUCHEZWA BILA YA MASHABIKI

admin September 11, 2021 8:43 am


 UONGOZI wa Klabu ya Yanga umethibitisha kuwa mechi yao ya kesho Jumapili dhidi ya Rivers United itapigwa bila ya uwepo wa mashabiki.

Ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo utachezwa Uwanja wa Mkapa. Jana Yanga walitoa taarifa kuhusu viingilio vya mchezo huo ila leo wametoa taarifa kwamba hakuna ruhusa ya uwepo wa mashabiki.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa CAF imezuia mashabiki kwa sababu Tanzania bado haijafikia viwango vya shirikisho hilo juu ya protokali za usimamizi wa ugonjwa wa Uviko-19.


Kwa mechi zote ambazo zitachezwa kwa wakati huu hazitakuwa na mashabiki ikiwa ni pamoja na ule wa leo wa Kombe la Shirikisho kati ya Azam FC dhidi ya Horseed FC ya Somalia.
Pia taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa imewasiliana na timu zote zinazoshiriki mashindano ya kimataifa ambazo ni Simba, Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Biashara United na Azam FC ambazo zinawakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho.
VIDEO: RATIBA YA LIGI KUU BARA IPO NAMNA HII, MECHI 15 NYUMBANI NA UGENINI KARIA, SIMBA, WATANZANIA WAMLILIA HANS POPE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply