news

HUYU HAPA AKABIDHIWA MIKOBA YA MUANGOLA WA YANGA

admin September 14, 2021 9:51 am


 KIUNGO mpya ndani ya kikosi cha Yanga, Jesus Moloko amekabidhiwa rasmi mikoba ya Carlos Carlinhos katika suala zima la kupiga mipira iliyokufa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.


Msimu uliopita Carlinhos raia wa Angola ambaye aliomba kusepa ndani ya kikosi cha Yanga alikuwa na jukumu la kupiga mipira iliyokufa na katika pasi zake tatu ambazo alitoa zote ilikuwa ni kwa mipira ya kona.

Juzi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 0-1 Rivers United nyota huyo alionekana akipipiga kona nyingi za Yanga jambo linalomaanisha kwamba mikoba ya Carlinhos kapewa nyota huyo.

Yanga ilipata jumla ya kona 7 katika mchezo huo na Moloko aliweza kupiga kona asilimia kubwa ikiwa ni ile ya dakika 37 ambayo ilileta kashikashi kwenye lango la Rivers United.

Licha ya Yanga kuweza kupata kona nyingi ambazo ni 7 huku wapinzani wao wakipiga kona moja walishindwa kutumia mapigo hayo huru jambo ambalo linawaongezea mzigo kuelekea kwenye mchezo wa marudio nchini Nigeria Septemba 18.  

BAADA YA ENZI ZA KAGERE KUISHA..SIMBA WAKOMAA NA MATIZI MAKALI KWA MUGALU..MWENYEWE AJIONGEZA.. HI HAPA ORODHA YA WACHEZAJI WA TP MAZEMBE WATAKAOCHEZA NA SIMBA,SEPTEMBA 19

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply