Azam FC

AZAM FC YATUSUA KIMATAIFA YASHINDA MBELE YA WASOMALI

admin September 18, 2021 4:43 pm


AZAM FC leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Horseed FC ya Somalia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ni bao la Isamil Kader alipachika bao pekee la ushindi dakika ya 38 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Horseed FC ya Somalia.

Mchezo wa leo kipindi cha kwanza Azam FC waliweza kupata ushindi huo na kipindi cha pili ngoma ilikuwa nzito kwa timu zote kuweza kupata bao.

Azam FC inasonga hatua inayofuata na itakutana na Pyramids FC katika mchezo wao ujao huku wapinzani wao Horseed FC wakigungashiwa virago.

Ushindi wa jumla ni Horseed FC 1-4 Azam FC. Vivier Bahati Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wanahitaji kufanya vizuri hatua inayofuata.

KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA HORSEED FC WIKI MOJA KABLA YA NGAO YA JAMII..GOMES AITANGAZIA MAAFA YANGA…AWATAJA TP MAZEMBE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply