Home news YANGA WAREJEA TANZANIA SALAMA KUTOKA NIGERIA

YANGA WAREJEA TANZANIA SALAMA KUTOKA NIGERIA


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Septemba 20 kimewasili salama katika ardhi ya Tanzania kikitokea nchini Nigeria.

Mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara walikuwa wakipambana kwa ajili ya kupeperusha bendera kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Deni lao kubwa ilikuwa ni kwenye kupindua meza kibabe mbele ya Rivers United kwa sababu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United hivyo walitakiwa kushinda mabao zaidi ya mawili.

Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Rivers United pia jana na mchezo ulipokamilika walianza safari kurudi Tanzania. 

Ni Shirika la Ndege la Tanzania walitumia ndege bora na wameweza kurudi salama Tanzania leo Septemba 20.


SOMA NA HII  BAADA YA KUONA WANAMCHELEWESHA.....ADEL ZRANE AANZA KUJIVUTIA SIMBA MWENYWE...