News

OMOG RASMI MALI YA MTIBWA SUGAR

admin September 24, 2021 6:43 pm


SASA ni rasmi, Joseph Omog raia wa Cameroon ni Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar ya Morogoro. 

Kocha huyo ametambulishwa leo Septemba 24 kwa mashabiki na wanachama wa Mtibwa Sugar.

Tayari leo ameanza kazi na vijana wake hao ambao kambi yao ipo Morogoro, mji kasoro bahari.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wanaamini kwa uzoefu alionao pamoja na uwezo ataifanya timu hiyo kuwa na ushindani mkubwa.

“Tunahitaji kufanya vizuri tofauti na msimu uliopita, uwepo wa Omog utatufanya tuwe na mwendo mzuri na matokeo chanya,”.

Kocha huyo amewahi kuinoa Simba pia na Azam FC hivyo ana uzoefu na Ligi Kuu Bara. 

SIMBA WAZIDI KUNEEMEKA…WAPATA UDHAMINI WA MABASI MAPYA ..WAPEWA MILIONI 800 KARIAKOO DABI, 2021 MWAKA WA REKODI SIMBA V YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply