kimataifa

WISSA MTIBUAJI WA MAMBO ULAYA

admin September 26, 2021 3:43 am


 YOANE Wissa, nyota wa Brenford alitibua shughuli ya Liverpool kusepa na pointi tatu mazima katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Brentford.

Katika mchezo huo uliokamilika kwa sare ya kufungana mabao 3-3, Liverpool ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kusepa na ushindi ila mambo yaligeuka ghafla na ngoma ikawa sare jambo lililofanya timu hizo kugawana pointi mojamoja.

Ni Diogo Jota dakika ya 31, Mohamed Salah dakika ya 54 na Curtis Jones alipachika bado dakika ya 67 kwa Liverpool huku yale ya Brentford yalipachikwa na Ethan Pinnock dakika ya 27,Vitaly Janelt dakika ya 63 na Wissa dakika ya 82.

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool ifikishe pointi 14 ikitofautiana pointi moja na Manchester City ambao waliibamiza bao 1-0 Chelsea, pia Manchester United wanapointi zao 13 walionyeshwa njia na Aston Villa kwa kutunguliwa bao 1-0 na Brentford ina pointi 9 ni baada ya kucheza mechi 6.


KERO ZA HAJI MANARA,OFISA HABARI WA YANGA NOMA KABISA MAKAMBO:SIMBA NI TIMU KUBWA, HAYA NI MATOKEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply