HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa kutokana na aina ya ubora wa wachezaji walionao ikiwa ni pamoja na Feisal Salum, Djuma Shaban wana imani kubwa ya kuweza kutwaa mataji ndani ya Tanzania.
Manara amesema kuwa watu wasiseme kuwa kikosi ni dhaifu kwa kuwa wameonyesha uwezo wao uwanjani.
Kuhusu malengo ameweka wazi kuwa ni kutwaa mataji yote yaliyobaki baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Rivers United.