News

YANGA:TUTATWAA MATAJI YOTE MSIMU HUU

admin September 27, 2021 5:43 pm


KAIMU Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amesema kuwa kushinda kwao Ngao ya Jamii ni mwanzo mzuri wa kwenda kutwaa makombe yote ya msimu huu.

 

Senzo alifunguka kuwa hakuna jambo nzuri kwa timu yoyote ile duniani kama kuanza msimu kwa ushindi au ubingwa na jambo nzuri kwao wameanza kwa kuifunga Simba ambao ni watani wao.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Senzo alisema kuwafunga Simba na kuchukua ubingwa ni kitu kikubwa kwao tofauti na watu wanavyofikiria kwa sababu hiyo itawaongezea morali na ari kuelekea kuanza msimu mpya wa ligi.

 

“Nafikiri hii sasa ni ishara ya kuwa makombe yote ya msimu huu ni ya kwetu, kumfunga Simba na kuchukua kombe ni jambo ambalo linatengeneza kitu cha utofauti kwenye timu.

 

“Watu wanajua kuwa hatuna mafanikio kwa misimu minne sasa, hivyo huu unakwenda kuwa msimu wa mataji kwa Yanga,” alisema Senzo.

 

Yanga waliwafunga Simba bao 1-0 na kutwaa Ngao ya Jamii kwenye mchezo ambao ulichezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa.

USIPANGE KUKOSA NAKALA YAKO YA GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE BALAA LA LEO UWANJANI LILIKUWA NAMNA HII, MATOKEO HAYA HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply