Ligi Kuu

HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO SEPTEMBA 28

admin September 28, 2021 7:43 am


SEPTEMBA 28, Ligi Kuu Bara inaendelea kuchanja mbuga baada ya jana Septemba 27 kuanza kasi kwa timu tatu kupambana kusaka pointi tatu. 

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu,  Didier Gomes itakuwa Uwanja wa Karume, Mara bila uwepo wa nyota wao Taddeo Lwanga ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa, Septemba 25.

Mbali na mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku kubwa pia Dodoma Jiji itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting,  Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. 

Pia kuna mchezo mwingine ambapo Mbeya City itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons,  Uwanja wa Sokoine.

BIASHARA UNITED WAIPIGA ‘PITI’ SIMBA…WATAMBA KUMALIZA MECHI MAPEMA TU ASUBUHI… ISHU YA NUGAZ KURUDI YANGA IPO HIVI, MANARA HANA TATIZO NAYE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply