News

YANGA YATUMA SALAMU GEITA GOLD

admin October 1, 2021 8:43 am


HAJI Manara Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa watapambana na Geita Gold kwa heshima licha ya kwamba imepanda daraja msimu huu.

Manara amesema baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao walifanikiwa kuondoka na alama  tatu kwa ushindi wa bao 1-0 wanaelekeza nguvu katika mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold. 

“Tunakwenda hatua kwa hatua,hatutasema sana zaidi ya hamasa kwa watu wetu.Mchezo wa  Kagera Sugar umepita, kwa sasa tunachoangalia  ni mchezo dhidi ya Geita Gold.

“Ni muhimu sana kwa kuwa ni mchezo wa kwanza nyumbani katika msimu huu. Haijalishi kwamba wamepanda daraja msimu huu lakini tunao wajibu wa kuwaheshimu kama timu ya ligi. Lakini wanapaswa kujua wanakuja kucheza na Yanga,” amesema Manara.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kipo Dar es salaam  tayari kuwakaribisha Geita Gold kesho kwa Mkapa.


RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO GEITA GOLD:TUNAWAHESHIMU YANGA ILA TUNATAKA POINTI TATU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply