news

HAJI MANARA:MASHABIKI WANAHITAJI SHUKRANI

admin October 5, 2021 10:43 am


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa shukrani nyingi lazima zirudi kwa mashabiki huku deni kubwa likiwa kwa wachezaji katika kutimiza majukumu yao.

Yanga inanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi hesabu zao ni kuweka kambi Arusha kipindi hiki cha mapumziko ili kuweza kupata muda wa kukijenga kikosi hicho ambacho kipo nafasi ya pili kwenye msimamo.

Mashabiki wa Yanga waliweza kuishuhudia timu hiyo ikisepa na pointi sita kwenye mechi mbili za ligi ikiwa ni ile iliyochezwa Uwanja wa Kaitaba na ubao ukasoma Kagera Sugar 0-1 Yanga na ule Uwanja wa Mkapa, Yanga 1-0 Geita Gold. 

Manara amesema:”Mashabiki ni watu muhimu wamekuwa wakiwapa nguvu wachezaji katika kupambana na wanapaswa shukrani,”.

Ameongeza kuwa kwa wakati huu Manara atakuwa anakaa eneo la mashabiki VIP B kuwapa sapoti na kuongeza nguvu ya kushangilia Yanga.

ORODHA YA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA WALIOANZA MAZOEZI JEMBE LA KAZI SIMBA LAANZA MAZOEZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply