Ligi Kuu

NBC WAFUNGUKA SABABU YA KUMWAGA MABILIONI LIGI KUU NA KUWA WADHAMINI WAKUU..

admin October 6, 2021 10:09 am


UBORA wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiyo chachu iliyopelekea Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kuingia kandarasi ya miaka mitatu na Shirikisho la Soka Tanzania TFF wa Sh2.5 bilioni kwa msimu mpya 2021/22.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa NBC, Teodas Sabi amesema, udhamini huo wa Sh2.5 bilioni kabla ya VAT itakuwa ni kwa ajili ya msimu huu mpya.

Amesema wameamua kuweka kiasi hicho cha fedha baada ya kujiridhisha ubora wa Ligi ya Tanzania kuwa nzuri.

“Mazungumzo yalikuwa ya muda mrefu sana, tumeridhika kabisa kuingia makubaliano na TFF tunatambua mpira wa miguu ndio mchezo pekee unaopendwa zaidi Duniani, “

Amesema mbali na hilo ubora wa Ligi umepelekea wachezaji wengi kuonekana na hata wa nchi jirani kutamani na kuja kucheza Tanzania.

NYOTA WATATU WATAJWA KUPIGWA STOP AZAM FC YANGA WATAMBA KUONGEZA MAKALI YA FISTON MAYELE, MAKAMBO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply