Home news TWIGA STARS WAREJEA TANZANIA NA TAJI LA COSAFA

TWIGA STARS WAREJEA TANZANIA NA TAJI LA COSAFA


MABINGWA wa taji la COSAFA, Timu ya Taifa ya Wanawake,’Twiga Stars’ leo wamerejea Tanzania wakitokea nchini Afrika Kusini ambapo walikuwa kwenye mashindano hayo.

Twiga Stars ilikuwa nchini Afrika Kusini ikiwa ni wageni waalikwa na wamefanya kweli katika mwaliko huo kwa kusepa na taji hilo.


 Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Bakari Shime mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julus Nyerere (JNIA) akiwa na msafara wa kikosi cha wachezaji wakitokea Afrika Kusini walikotwaa ubingwa wa COSAFA Wanawake 2021 amesema kuwa yalikuwa ni malengo kufanya vizuri.

“Tumeweza kufanya kile ambacho tulikuwa tunahitaji kufanya kwa kuwa tulikwenda kushiriki na malengo ilikuwa ni kuweza kufanya vizuri jambo ambalo limetokea.

“Tulikuwa tunajua kwamba ushindani utakuwa mkubwa na imekuwa hivyo, tumejifunza na tumepata kitu kutoka kwenye mashindano hayo,” amesema.

Pia kabla ya kurejea kutoka Afrika Kusini wachezaji na benchi la Ufundi la Timu ya Taifa ya Wanawake waliweza kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kumtembelea.

SOMA NA HII  SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA LATINGA IKULU...RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO KWA INJINIA HERSI...