news

KIPA MPYA SIMBA MAMBO BADO

admin October 13, 2021 11:43 am


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kipa wake Jeremia Kisubi bado anahitaji muda ili kuweza kufanya vizuri.

Kisubi kwa sasa yupo ndani ya kikosi hicho ambacho kinafanya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Gomes amesema anatambua uwezo wa nyota huyo na amekuwa akifanya vizuri kwenye mazoezi lakini bado kuweza kuanza katika kikosi cha kwanza kwa kuwa hajawa imara.

“Kisubi ni kipa mzuri lakini bado hajawa imara kwa sasa kwa sababu alikuwa anaumwa kwa muda mefu na wakati huu anaendelea na mazoezi.

“Jambo ambalo linasubiriwa kwake ni kuwa katika hali yake ya kawaida na hiyo itafanya tuwe na chaguo kubwa kwenye upande wa makipa,”.

KISA LAWAMA ZA KUSHINDA GOLI MOJA MOJA…MAYELE AAMUWA KUWAPA ‘MAKAVU’ MASHABIKI YANGA BAADA YA KUKOSA MECHI MBILI ZA LIGI KUU..KANOTE AIBUKA NA HAYA…ATAJA VIWANJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply