KMC FC

KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA….KMC YAWATENGEA MAMILIONI WACHEZAJI..

admin October 16, 2021 8:04 am


MABOSI wa KMC wamepiga hesabu za haraka kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa Oktoba 19 katika Uwanja wa Majimaji.

Katibu Mkuu wa KMC, Walter Harrison amesema wameamua kuondoka jana Ijumaa kwa ajili ya wachezaji kupata muda mzuri wa kupumzika kabla ya mchezo huo.

Akizungumzia mchezo huo, alisema hakuna mambo makubwa wanayoweza kuwaahidi wachezaji wao, lakini huwa kuna bonasi kila mchezo ambao wakishinda hupatiwa.

“Kuna bonasi zetu maalumu ambazo zipo kwa kawaida kwenye kikosi. Maandalizi ni mazuri kwenye mchezo huu na vijana wana morali kubwa. Huwa tunazungumza nao karibu kila mchezo na kuwaambia umuhimu wa pointi tatu,” alisema Walter.

Soka la Bongo limefahamishwa kwamba kwa mechi kama ya Yanga timu nzima hupewa Sh3 milioni, ingawa siku ya mchezo ahadi huongezeka kutoka kwa viongozi mbalimbali. Kama itabaki hiyo tafsiri yake ni kwamba kila mchezaji atapata posho ya Sh150,000.

Walter licha ya kufanya siri, alisema wao kama uongozi wanatambua ugumu wa mchezo huo, lakini anaamini kwa namna ambavyo usajili wamefanya watakuwa vizuri kwenye msimu huu wa ligi kila mchezo.

WAKITUA SALAMA BOTSWANA..KIGOGO AFICHUA SABABU ZA SIMBA KUTOPANDA NDEGE ZA ATCL BAADA YA KUTUA RUVU SHOOTING…ALLY SONSO ASIMULIA ALIVYOFUKUZWA YANGA..AMTAJA ZAHERA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply