News

SIMBA KUANZA ‘TIZI’ LA KUWASAMBARATISHA MAZIMA WABOTSWANA KESHO

admin October 19, 2021 8:00 pm


Mabingwa wa Tanzania Bara na Wawakilishi wa Ligi ya Mabingwa Simba SC, kesho wataanza mazoezi rasmi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi Ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Kikosi cha Simba SC kilirejea jana Jumatatu (Oktoba 18) kikitokea Gaborone, Botswana ambako walicheza dhidi ya Jwaneng Galaxy Jumapili (Oktoba 17), na leo Jumanne (Oktoba 19) wachezaji walikuwa mapunziko.

Simba SC inajiandaa na mchezo wa mkondo wa pili, huku ikikumbuka ushindi wa mabao 2-0, mjini Gaborone.

Mabao wa Simba SC katika mchezo huo yalifungwa na Nahodha na Mshambuliaji John Bocco dakika ya 02 na 05.

Mchezo wa mkondo wa pili utachezwa Jumapili (Oktoba 24), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

MWAMNYETO :- TULIHIMIZWA KUWAFANYIA KITU KMC DAKIKA 15 ZA KWANZA BAADA YA KUWACHACHAFYWA WABOTSWANA KWAO..GOMES AIOTA NUSU FAINAL LIGI YA MABINGWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply