news

WALICHOKIFANYA YANGA KWENYE MSIBA WA BABA YAKE PAUL GODFREY CHAWEKA HISTORIA TZ

admin October 20, 2021 1:36 pm

 


Saa chache baada ya kutua jijini Dar es salaam wakitokea Songea mkoani Ruvuma, Wachezaji wa Young Africans walifika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kuaga mwili wa Baba Mzazi wa Beki wa kulia wa klabu hiyo Paul Godfrey ‘Boxer’.

Mzee Godfrey Nyang’anya alifikwa na umauti siku moja baada ya kikosi cha Young Africans kuwasili mjini Ruvuma mkoani Songea, kwa ajili ya mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC FC.

Kwa majonzi makubwa wachezaji wa Young Africans walifika Hospitali ya Temeke ikiwa ni sehemu ya kumfariji mchezaji mwenzao, ambaye alilazimika kurejea jijini Dar es salaam.

Mbali na Wachezaji, pia baadhi ya viongozi wa Young Africans walijumuika na Mfiwa hispotalini hapo.

Young Africans jana Jumanne (Oktoba 19), ilicheza dhidi ya KMC FC mjini Songea mkoani Ruvuma katika Uwanja wa Majimaji, na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

BAADA YA KUIONA SIMBA ILIVYOCHEZWA BOTSWANA..EDO KUMWEMBE AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA KIKOSI CHA WACHEZAJI 25 WA AZAM FC CHAIFUATA PYRAMIDS YA MISRI KIBABE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply