CAF

WABOTSWANA WAIFANYIA SIMBA UMAFYA WAKIWA TZ..SIMBA WASHUTUKIA TAYARI MCHEZO UMEISHA

admin October 21, 2021 4:00 pm

 


WALICHOKIFANYA Jwaneng Galaxy ya Botswana ni kama umafia kwa Simba kwani wameamua kutua Dar kimyakimya bila ya wenyeji wao kuwa na taarifa.

Waswana hao ambao wikiendi iliyopita wakiwa kwao walikubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Simba, wameamua kufanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kutaka kupindua meza.

Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, Simba itaikaribisha Jwaneng ukiwa ni mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza ambapo mshindi wa jumla atafuzu makundi.Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja Maudhui wa Simba, Ally Shatry ‘Babu Chico’, alisema wamepata taarifa za ghafla kuwa tayari wapinzania wao wapo nchini, jambo lililowashtua kutokana na kuingia kimyakimya, wakati wao walikuwa tayari kwa ajili ya kuwapokea kama wenyeji.

“Tumepata taarifa za kushangaza kidogo asubuhi hii (jana Jumatano), ambapo tumetaarifiwa kuwa wapinzani wetu Jwaneng Galaxy tayari wameingia nchini kinyemela na wamefikia White Sands Hotel.

“Kiukweli sisi kama wenyeji wao tumeshtushwa na taarifa hizo, maana utaratibu tulijua tutawapokea na kuwaandalia sehemu sahihi ya kufikia, lakini mambo yameenda sivyo, hivyo sisi tunawakaribisha ila wafahamu kipigo kipo palepale,” alisema Chico.

BAADA YA CAF KURUHUSU MASHABIKI…WABOTSWANA WAINGIA HOFU DAR…KOCHA WAO AFUNGUKA HUKU SAIDO AKIWA HAJUI HATMA YAKE YANGA…KAZE IBUKA NA HILI KUHUSU MAYELE..AMTAJA FEI TOTO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply