Home BIashara United BIASHARA UNITED YAWAVUTIA KASI AL AHLY TRIPOLI

BIASHARA UNITED YAWAVUTIA KASI AL AHLY TRIPOLI


WANAJESHI wa mpakani, Biashara United,  leo Oktoba 13 imeendelea kuwavutia kasi wapinzani wao katika mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Itakuwa ni Oktoba 15 Ijumaa dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa nchini Libya.

Wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Biashara United,  Seleman Mataso amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya.

SOMA NA HII  HUU HAPA UNDANI WA AJALI YA FEI TOTO JANA AKIWA ZNZ....POLISI WAANIKA KILA KITU A-Z...