Home news POLISI TZ:- HUYU MORRISON SIO POA KABISA …WAFUNGUKA ALICHOWAFANYIA UWANJANI…CAF YAHUSISHWA

POLISI TZ:- HUYU MORRISON SIO POA KABISA …WAFUNGUKA ALICHOWAFANYIA UWANJANI…CAF YAHUSISHWA

 


MASTAA wa Polisi Tanzania wameangalia uwezo wa Simba ndani ya dakika 90, wakamtaka kwamba Bernard Morrison ni mtu muhimu anayepaswa kupewa muda mwingi wa kucheza kwani ana madhara.

Wamesisitiza kwamba kwa Simba kwa hali waliyonayo sasa wanahitaji wachezaji machachari aina ya Morrison hata watatu ili kurejea kwenye makali yao na hata kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Kwenye mechi ya juzi ambayo Polisi ililala bao 1-0, Morrison aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kibu Denis na kusababisha penalti ya ushindi. Beki tegemeo wa Polisi Tanzania alimtaja Morrison kama mchezaji mjanja wa kuitafutia timu yake matokeo na kwamba laiti kama watapatikana wachezaji watatu kama yeye, upepo utabadilika. “Kuingia kwa Morrison kuliichangamsha safu ya ushambuliaji na ndiye aliyesababisha wapate penalti,anajua sana,”alisema.

Kipa wa Polisi, Metacha Mnata alisema; “Nimecheza michuano ya Caf, najua ushindani wake ulivyo mkali, wachezaji wa Simba wanapaswa kuongeza jitihada kwa ajili ya michuano ya Shirikisho, timu ina wachezaji wazuri ila warudi mchezoni.”

Ukiachana na wachezaji wa Polisi Tanzania,mchezaji wa zamani wa Simba, Shaban Kisiga alisema endapo kama wachezaji wataamua kuhamasishana na kupeana moyo watarejea kwenye ubora.

“Wasiyachukue maneno ya mashabiki vibaya, kwani wanajua wachezaji hao wana kiwango cha juu, hawajafanya pale wanapotakiwa wawe, wakaze buti watafika tu,”alisema.

Makapu aliongeza kuwa hakuona mashuti makali ya washambuliaji yaliyomsumbua na aligundua walikosa utulivu, aliyowashauri wautafute kabla ya mechi yao ya Shirikisho.

“Licha ya kufungwa bao la penalti, Simba ilisumbuka sana kusaka pointi tatu, hilo linatoa taswira ya kazi ngumu wanayotakiwa kuifanya michuano ya Caf, kwani huko wanakutana na ushindani zaidi ya huu,”alisema Makapu na aliongeza kuwa;

“Sikuuona muunganiko mzuri wa Simba, bado inahitaji kutengenezwa zaidi kurejea kwenye ushindani waliokuwa nao misimu minne iliyopita, ila kwa haraka haraka wanapaswa kupandisha morali yao ya kazi iwe juu,”alisema. Simba imerudi kambini jana jioni kujiandaa na Coastal.

SOMA NA HII  WAWA AVUNJA UKIMYA SIMBA...AANIKA WAZI MAHUSIANO YAKE NA PABLO..ATAJA TOFAUTI ZAO..