Home news ZA UHAKIKA…BAADA YA KUWABAMIZA AZAM JANA..SIMBA WAMMEZEA MATE NABI…YANGA WATOA TAMKO..

ZA UHAKIKA…BAADA YA KUWABAMIZA AZAM JANA..SIMBA WAMMEZEA MATE NABI…YANGA WATOA TAMKO..


IMEELEZWA kuwa, licha ya Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, kuachia nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, lakini bado anahusika kwenye baadhi ya mambo ikiwemo kipindi hiki cha mchakato wa kusaka kocha mpya wa kuinoa timu hiyo.

Wakati Simba ikiwa kwenye mchakato wa kumsaka mrithi wa Kocha Didier Gomes aliyeachia ngazi Jumanne ya wiki hii, baadhi ya viongozi wa Simba wameonekana kulijadili jina la Kocha wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka Simba, viongozi wa timu hiyo wamekuwa bize kwenye vikao juu ya kuangalia nani atakuwa kocha sahihi wa kurithi mikoba ya Gomes.

Mtoa taarifa huyo alieleza kwamba, katika mjadala wa kumpata mrithi wa Gomes, wapo waliolitaja jina la Nabi kutokana na kuhitaji kocha ambaye anayajua mazingira ya soka la Tanzania, lakini pia mwenye uzoefu wa michuano ya kimataifa.

“Ndugu yangu suala la kupata kocha mpya limechukuliwa sura tofauti sana na Mo, kwani aliomba kupewa mapendekezo ya kocha anayestahili, wengi walimtaja Nabi ambaye anaonekana ufundishaji wake unaendana na matakwa yetu.

“Mazungumzo baina ya viongozi na Nabi yanaweza kufanyika muda wowote kuanzia sasa, shida wanaangalia namna gani ataweza kuachana na timu yake ya sasa, lakini kama mambo yataenda vizuri, basi atachukua mikoba ya Gomes,” kilisema chanzo hicho.

Spoti Xtra lilimtafuta Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said ili kuzungumzia kama wamezipata taarifa za kocha wao kutakiwa upande wa pili na kama wapo tayari kumuachia endapo ishu hiyo ikiwa kweli.

Alipopatikana, Injinia Hersi alisema: “Hakuna taarifa kama hiyo kwetu ingawa naamini wazi kabisa hakuna kocha anayeweza kukaa sehemu moja milele.

“Ila kwa taarifa hii, sidhani kama inawezekana mtu yoyote kumchukua kocha wetu hasa wakati huu ambao timu ina malengo makubwa ya kufika mbali. Sitaki kuonekana nabisha ila ukweli ni kwamba haiwezekani Nabi kwenda Simba kwa sasa.”

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUWEKWA KUNDI MOJA NA TIMU YA CHAMA...PAWASA ATIKISA KICHWA..AFUNGUKA HAYA...