News

PAMOJA NA KUSHINDA…MASTAA YANGA WASHINDWA KUJIZUIA..WAFUNGUKA KUHUSU NABI NA MBINU ZAKE…

admin November 5, 2021 4:00 pm

 


NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amefunguka kuwa kwa sasa nyota wa kikosi hicho wanafurahia zaidi mfumo wa soka la pasi nyingi, ambao unafundishwa na kocha mkuu Nasrredine Nabi, kulinganisha na utamaduni wao wa awali wa kutumia mipira mirefu.

Tangu msimu huu umeanza kocha Nabi anaonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibadilisha Yanga ambayo sasa inacheza mpira wa pasi nyingi, tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakitumia mipira mirefu.

Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa wakiwa na asilimia 100 ya ushindi ambapo wamefanikiwa kujikusanyia pointi 15, katika michezo mitano waliyocheza mpaka sasa.

Akizungumza na Gazeti la  Championi Ijumaa, Mwamnyeto alisema: “Ni jambo zuri kuona tumeuanza msimu huu kwa matokeo mazuri ambapo mpaka sasa tunaongoza msimamo, najua kila mmoja anaona mabadiliko makubwa ya kiuchezaji jambo ambalo kama wachezaji tunalifurahia zaidi.

“Hatukuwa na muda mrefu wa maandalizi ya kabla ya msimu, lakini kocha amefanya kazi kubwa kutengeneza muunganiko wa kikosi ambao unaleta matokeo mazuri na soka la kuvutia.

BAADA YA AJIBU ‘KUKIWASHA’ JUZI DHIDI YA NAMUNGO…ZAHERA AIBUKA NA HILI…ADAI AJIBU NI MVIVU MNOO… MCHAKATO KOCHA MPYA SIMBA WAFIKIA PATAMU…KUTANGAZWA NDANI YA SIKU 14….SIRI YAFICHULIWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply