Singida Black Stars
Michezo Soka la Bongo

Mastaa Singida Black Stars Kuti Kavu: Dirisha Dogo Laleta Maumivu!

Vardo November 11, 2026 9:10 pm

HALI si shwari kwa mastaa wa Singida Black Stars! Kikosi hicho kinatajwa kuwa kwenye wakati mgumu kufuatia uamuzi wa benchi la ufundi kuanza mchakato mkali wa kupima viwango vya wachezaji wote, huku panga zito la usajili likitajwa kuwakabili wengi kuelekeza dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Januari 2027.

Taarifa za ndani kutoka klabuni hapo zimethibitisha kuwa wachezaji waliokalia kuti kavu ni wale watakaoshindwa kuonyesha uwezo wa kuridhisha kuanzia sasa, huku tathmini ya kina ikiwa chini ya uangalizi wa karibu wa kocha mkuu raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo), Papy Kimoto.

Akizungumzia hali hiyo, chanzo cha kuaminika kilieleza kuwa benchi la ufundi limepewa mamlaka kamili ya kumchunguza mchezaji mmoja mmoja ili kuona kama wanaendana na malengo na ushindani wa kikosi hicho msimu huu.

“Hadi kufikia usajili wa dirisha dogo Januari 2027, tutakuwa tumefikia uamuzi wa mwisho. Tathmini tumeianza mapema na tunazingatia zaidi mechi za Ligi Kuu na hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika,” kilisema chanzo hicho.

Utaratibu Unauma, Vigogo Waomba Kuvunja Mikataba

Mchakato huu mkali umeanza kuleta mabadiliko ya haraka kikosini, ambapo baadhi ya wachezaji wameamua kuomba wenyewe kuvunja mikataba yao kutokana na hofu ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, alithibitisha kuwa mabadiliko hayo yanatokana na mahitaji halisi ya timu na viwango vya ushindani uliopo.

Baadhi ya nyota ambao tayari wametemwa au kufikia makubaliano ya kusitisha mikataba yao ni pamoja na:

  • Marcel Canadi (Kiungo kutoka Austria, aliyetokea Enosis Neon Paralimni ya Cyprus)

  • Mohamed Damaro (Kutoka Guinea)

  • Ladack Chasambi (Winga mahiri)

  • Dramane Kambou (Raia wa Burkina Faso aliyetokea FC Saint-Eloi Lupopo ya DR Congo)

Wakati ushindani ukiendelea kuwa mkali ndani ya kikosini, mashabiki wa Singida Black Stars wanatazamia kuona sura mpya zenye tija zitakazotua kikosini hapo kusaidia kupambana kwenye michuano ya ndani na kimataifa.

Krismasi Yenye Baraka Za Big Bass Christmas Blast 1000 Ipo Meridianbet