News

HUKU AKIWA BADO WA ‘MOTO MOTO’….MOLOKO AJIPA KAZI YA KUMNG’ARISHA MAYELE….

admin November 9, 2021 7:00 pm


WINGA ya Yanga, Jesus Ducapel Moloko, amesema atahakikisha anaongeza juhudi katika kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao wakiongozwa na Fiston Mayele ili yapatikane mabao mengi.

Moloko amejiunga na Yanga msimu huu akitokea AS Vita ya DR Congo ambapo mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu Bara amefanikiwa kufungia mabao mawili katika mechi tano, huku akiwa hana asisti.

Akizungumza na  Gazeti la Spoti Xtra, Moloko aliweka wazi matanio yake ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenda katika idara ya ushambuliaji huku akisema atahakikisha anaongeza juhudi kufanikisha hilo.

“Katika nafasi ambayo nacheza vitu vya msingi kwangu ni kutengeneza mabao pamoja na kufunga, tayari nimefanikiwa kutimiza moja lakini lingine bado sijafanikiwa.

“Natakiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi kwenda kwa washambuliaji ili waweze kufunga mabao ya kutosha, natamani kuona hilo nilikifanya.

“Bado kuna michezo mingi, nitapambana kuhakikisha safu ya ushambuliaji nawapikia mabao ya kutosha, nafahamu haitakuwa kazi nyepesi, lakini nitapambana kuhakikisha nafanikiwa,” alisema winga huyo raia wa DR Congo.

YANGA KWISHA HABARI YAKE…KOCHA MPYA SIMBA ‘APEWA MKANDA’ MZIMA…SASA MPANGO MPYA UKO HIVI… TAJIRI GSM AWAPA MASTAA YANGA NYUMBA…HITIMANA ASIMULIA ALIVYOPITIA MAGUMU SIMBA…CHAMPION..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply