Home news YANGA WAZIDI KUIGHARAGAZA SIMBA KILA KONA…MASUDI DJUMA AFUGUKA ISHU NZIMA ILIVYO..

YANGA WAZIDI KUIGHARAGAZA SIMBA KILA KONA…MASUDI DJUMA AFUGUKA ISHU NZIMA ILIVYO..


SEMA yote lakini takwimu zinasema kiungo cha Yanga msimu ni ghali kuliko Simba. Pale wanaposimamaga Khalid Aucho, Yanick Bangala na Feitoto.

Katika kikosi cha Simba kuna Thadeo Lwanga aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo msimu uliopita mkataba wa miaka miwili na nusu ambao ulikuwa na thamani ya Dola za Kimarekani 45,000 ambazo kwa pesa za Kibongo ni zaidi ya Sh90 milioni.

Msimu huu Simba wamemsajili Sadio Kanoute ambaye alivuta Dola 60,000 ambazo ni zaidi ya Sh120 milioni, wakati dirisha moja nyuma walimsajili Bwalya kwa Dola 50,000 ambazo ni zaidi Sh100 milioni na wakaja kumuongezea mkataba wa miaka miwili kwa Sh50 milioni.

Viungo hao watatu tegemeo wa kikosi cha kwanza Simba ndani ya madirisha mawili ya usajili wamevuta zaidi ya Sh360 milioni.

Huko kwa jirani zao Yanga, katika kikosi cha kwanza msimu huu kuna viungo watatu tegemeo ambao wamekuwa wakicheza vizuri tena kwa maelewano makubwa katika mechi zote za kimashindano.

Viungo hao ni Yannick Bangala na Khalid Aucho ambao wanacheza katika nafasi ya ukabaji pamoja na Feisal Salum ambaye hucheza katika nafasi ya kiungo mshambuliaji na amekuwa katika kiwango bora msimu huu.

Taarifa zinasema kwamba Bangala  alivuta Dola 70,000 ambayo ni zaidi ya Sh140 milioni wakati Aucho Dola 120,000 ambayo ni zaidi ya Sh276milioni na wawili hawa wamesajiliwa msimu huu.

Feisal msimu uliopita aliongeza mkataba wake na kuwa wa miaka mitatu mbele na alivuta Sh90 milioni kutoka kwa vinara hao wa ligi ambao msimu huu wameonyesha kuwa na kiu ya kutwaa ubingwa baada ya kulikosa taji kwa miaka minne.

Bangala, Aucho na Feisal watatu hao ndani kiujumla wamevuta zaidi ya Sh500 milioni kama thamani ya usajili wao, ambao umeonekana kulipa msimu huu kutokana na viwango vyao kuwa bora.

Miongoni mwa eneo lenye wachezaji wengi katika vikosi vya Simba na Yanga ambao wanafanya vizuri ni katika kiungo na hata wakikutana ushindani unakuwa wa aina yake.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Katika kikosi cha kwanza Simba msimu huu wametumika zaidi viungo hao wanne tofauti na Yanga ambao wao wamekuwa wakitumia zaidi viungo watatu hao wawili wakabaji na mmoja mshambuliaji.

Kikosi cha kwanza Simba mbali na Lwanga ambaye kwa sasa ni majeruhi, Sadio Kanoute, Larry Bwalya kuna Hassan Dilunga.

Kocha wa AS Kigali ya Rwanda, Masoud Djuma alisema miongoni mwa eneo ambalo Yanga wamefanikiwa msimu huu ni hapo kwenye kiungo Bangala na Aucho wameongeza ubora wa kikosi hicho.

“Sina shaka na ubora wa Feisal kwani tangu nikiwa Simba niliwahi kumtaka tena wakati huo hafaamiki ila tulishindwa kutokana na sababu fulani hivi na timu yoyote ambayo inahitaji kufanya vizuri lazima iwekeze kama hivyo,” alisema Djuma na kuongeza;

“Binafsi Yanga wamestahili kutoa pesa hiyo kutokana na ubora wa wachezaji hao lakini kwa msimu msimu huu binafsi bado wanakazi ya kufanya ili kuonyesha uimara katika eneo lao la kiungo pengine kama msimu uliopita.”

Kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael alisema Simba bado wameimarika kwani kuondoka kwa wachezaji wawili si tatizo ila wapya ambao wameingia msimu huu ndio wanatakiwa kuonyesha thamani ya pesa ya usajili iliyotumika kwao.

“unaweza kutumia pesa nyingi katika usajili na wachezaji wakashindwa kufanya vizuri lakini unaweza kutumia kidogo na wakafanya vizuri kwahiyo niwapongeze Yanga ya msimu huu ni imara tofauti na wakati naifundisha,” alisema Eymael.