news

KISA AUCHO KUCHEZESHWA NAFASI YAKE…MUKOKO ASHINDWA KUJIZUIA..AIBUKA NA JIPYA KUHUSU UWEZO WAKE..

admin November 15, 2021 10:00 am


KIUNGO wa Yanga raia wa DR Congo, Mukoko Tonombe, ameahidi kufanya mazoezi mazito ili aweze kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

Mukoko msimu huu amekuwa na wakati mgumu wa kucheza kikosi cha kwanza kutokana na kupata upinzani mkali mbele ya Mganda, Khalid Aucho.

Katika mechi tano za Ligi Kuu Bara msimu huu, Mukoko amecheza moja, huku Aucho akicheza nne ambapo Kocha Nasreddine Nabi, eneo la kiungo amekuwa akiwatumia zaidi Yanick Bangala, Feisal Salum na Aucho, huku Zawadi Mauya na Mukoko wakisubiri.

Akizungumza na hivi karibuni, Mukoko amesema: “Natamani sana ligi ikiendelea nipate nafasi ya kucheza ili nifanikishe lengo langu la kuchukua Tuzo ya Mchezaji Bora msimu huu.“Nitajitahidi kufanya mazoezi makali ili tu niweze kupata nafasi mbele ya viungo wenzangu ambao kwa sasa wanaaminiwa na kocha.”

KWA SIMBA HII YA KOCHA MHISPANIA…LITAKUFA JITU WALAH…AURUDISHA MFUMO WA MASOUD DJUMA.. SIKU CHACHE BAADA YA KUFUKUZWA …ADEL ZRANE AIBUKA NA KUFICHUA YA SIMBA…AGUSIA USAJILI …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply