news

KINDA LA KITANZANIA LASAJILIWA NA TIMU TAJIRI YA SUDANI…INASHIRIKI LIGI YA MABINGWA AFRIKA…

admin November 17, 2021 12:21 pm

 


Mtanzania ambaye ni winga chipukizi, David Richard Ulomi amejiunga na mabingwa wa Sudan, Al Hilal kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Dodoma Jiji FC ya jijini Dodoma.

Al Hilal wamefanikiwa kufuzu hatua za makundi ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, kwa upande wa Ulomi Mafanikio hayo yanakuja ikiwa ni hivi karibuni alijiunga na Dodoma Jiji FC akitokea katika timu ya Ruvu Shooting.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 16, 2021 na Idara ya Habari na Uhusiano ya Dodoma Jiji FC imeeleza kuwa, timu hiyo imeridhia kwa kauli moja makubaliano hayo.

“Klabu yetu inapenda kuwajulisha wanahabari, mashabiki wetu na wapenzi wa soka kwa ujumla kuwa, tumefikia makubaliano ya uhamisho ya mchezaji David Richard ulomi kujiunga na Klabu ya Al Hilal inayoshiriki Ligi Kuu nchini Sudan.

“Klabu yetu inatoa shukurani za kipekee kwa mchezaji david Ulomi kwa mchango wake mkubwa kwenye timu yetu na tunamktakia kila lenye heri katika majukumu yake mapya,” imeeleza taarifa hiyo.

HIZI HAPA TIMU KUMI ZA AFRIKA ZILIZOFUZU HATUA YA MTOANO KOMBE LA DUNIA QATAR.. MBADALA WA MIQUISSONE AREJEA SIMBA…HITIMANA NI FULL SHANGWE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply