news

PABLO AANIKA TATIZO LA KWANZA SIMBA…HITIMANA KAMA KAWA ADAKIA…WAWA, DILUNGA WAJIIONGEZA…

admin November 18, 2021 10:00 am


KOCHA wa Simba, Pablo Franco amewaambia viongozi kwamba ishu ya kwanza kwenye timu ni fiziki kwani amebaini kwamba ipo chini na inahitaji kufanyiwa kazi kwa nguvu.

Katika kuhakikisha hilo amewaambia pia wachezaji kila mmoja afanye programu za ziada za ndani na nje ya uwanja kwa haraka sana ili kwenda na kasi yake.

Lakini katika kutekeleza hilo, wachezaji wawili wamemuelewa fasta wakaamua kujiongeza wenyewe ambao ni Pascal Wawa na Hassan Dilunga.

Wachezaji hao tangu Kocha huyo aanze programu zake wameomnyesha kujituma kwa hali ya juu na kufanya mambo mengi ya ziada. Kocha Thiery Hitimana aliweka wazi hivikaribuni kwamba walikaa na Wawa na akamueleza kwamba hakufanya vizuri kimataifa hivyo atalazimika kukaa benchi ajitathmini upya. Dilunga yeye amekuwa hapati namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Simba mikononi mwa makocha kadhaa.

Inafahamika  kwamba Pablo tayari ameshakaa na wasaidizi wake, Seleman Matola na Thiery Hitimana na kuwaeleza pia wachezaji kama hawako kambini lazima wakutane kwanza tofauti na utaratibu alioukuta wa watu kupitiliza moja kwa moja mazoezini Bunju.

Katika mazoezi yaliyofanyika chini yake wiki hii inaelezwa amekuwa akisisitiza uharaka wa kila jambo mchezaji anapokuwa uwanjani na hataki mzaha wowote au kumuona mtu anatembea tu.

HITIMANA: JAMAA ANAJUA

Hitimana alisema kikosi chao kwa sasa hakina wachezaji wengi waliokuwa katika timu inayocheza mechi shindani wengi ni wale kutoka katika timu ya vijana.

Hitimana alisema anadhani akipata muda zaidi wa kukaa na Franco ataelewa mambo mengi kutoka kwake haswa wakiwepo na wale wachezaji waliokuwepo katika timu ya taifa wakati huu.

β€œKuna vitu vizuri kutoka kwake kwa muda huu mfupi tuliokuwa nae anamalengo makubwa kuona Simba inafanya vitu ambavyo vitakuwa silaha ya kufika mbali na kufikia mafanikio,” alisema Hitimana na kuongeza;

β€œWasaidizi wake tupo tayari kumpatia ushirikiano katika falsafa zake na kile ambacho anahitaji katika timu ili kuona malengo ya klabu tunayafikia.”

WAKATI MAKAMBO AKIWA BADO ‘USINGIZINI’ KWENYE KUFUNGA..NABI AMALAZIMISHA HAYA MAYELE… KUELEKEA MECHI  DHIDI YA RUVU…..KAPOMBE AKIRI UBOVU SIMBA…ATOA AHADI MECHI YA KESHO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply