news

KUELEKEA MECHI DHIDI YA RUVU…..KAPOMBE AKIRI UBOVU SIMBA…ATOA AHADI MECHI YA KESHO….

admin November 18, 2021 11:00 am


BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amekiri timu yao kuanza vibaya msimu huu na kuahidi mabadiliko makubwa kuanzia Ijumaa.

Simba inatarajia kushuka uwanjani CCM Kirumba Mwanza kumenyana na Ruvu Shooting ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 waliyoshinda katika uwanja huo msimu uliopita.

Kapombe amesema wameanza vibaya lakini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kusawazisha makosa yao kabla ya mchezo wao wa Ijumaa na kuwaahidi mashabiki wao furaha.

“Tupo imara ukiachana na majeruhi waliopo kikosini Simba ina kikosi kipana wachezaji tuliopo tunatosheleza kufanya vizuri kwenye michezo yote iliyo mbele yetu sio Ruvu Shooting pekee,” alisema na kuongeza kuwa.

“Simba tunakubaliana na kila hari lakini hatujawahi kukata tamaa kwa kuamini kuwa hatuwezi malengo yetu ni kutetea ubingwa tumejiandaa kwaajili ya ushindani kila mechi kwetu ni fainali,” alisema.

PABLO AANIKA TATIZO LA KWANZA SIMBA…HITIMANA KAMA KAWA ADAKIA…WAWA, DILUNGA WAJIIONGEZA… IKIWA KESHO SIMBA INAKIPIGA NA RUVU…KAMA KAWA AJIBU ABAKISHWA DAR..PABLO AFUNGUKA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply