News

MKUTANO MKUU SIMBA: MH ZUNGU ATUPA DONGO YANGA…AMTAJA NYERERE…BARBARA APAISHWA…

admin November 21, 2021 8:39 am


Mussa Azan Zungu ni kama ameipiga kijembe Yanga kwenye hotuba yake katika mkutano mkuu wa klabu ya Simba unaoendelea Dar es Salaam.

Zungu ambaye ni mgeni rasmi kwenye mkutano huo alitumia dakika 15 kuzungumza na moja ya vitu alivyozungumza ni kwamba baadhi ya watu wanaamini timu yao ndiyo ilishiriki kwenye uhuru wa Tanganyika.

“Hao hawajui historia ya nchi yetu, eti klabu yao imeshiriki kwenye uhuru,” alitania Zungu huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wa klabu hiyo.

Amesema viongozi waandaamizi wa Serikali akiwamo, aliyekuwa waziri mkuu, Rashid Mfaume Kawawa walikuwa ni wanachama wa klabu hiyo walioshirikiana ipasavyo na Mwalimu Nyerere.

“Wacha wajisifu tu, lakini Taifa letu ni moja na mwenyezi Mungu ni mmoja, lakini hawafahamu historia,” amesema Zungu.

Katika hotuba yake pia ameupongeza uongozi wa klabu hiyo na Ofisa mtendaji mkuu, Barbara Gonzalez.

“Maneno yalikuwa mengi ulipoteuliwa kuwa CEO, lakini umeonyesha unaweza na sasa wewe ni CEO uliyekubuhu, usiogope vijembe na maneno hayo yapo tu,” amesema.

JINSI VITENDO VYA ‘KISHOGA’ VINAVYOZIDI KUSHAMIRI KWENYE LIGI KUU..WACHEZAJI , VIONGOZI WATAJWA… BREAKING NEWS: MO DEWJI APEWA URAIS SIMBA…WANACHAMA FULL KICHEKO..TRY AGAIN ASANUKA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply