news

BAADA YA KUSHINDWA NA MORRISON..YANGA WABADILI GIA ANGANI… WAIBUKA NA HILI JIPYA…

admin November 24, 2021 8:39 am


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa tayari umemlipa kiungo wao zamani Mghana, Bernard Morrison faini ya Sh 12Mil kutoka Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ‘CAS’ huku ukiwataka mashabiki wa timu hiyo kupotezea majibu ya hukumu hiyo.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu CAS itangaze hukumu ya Morisson na Yanga ambayo ilishindwa huku ikitakiwa kumlipa kitita cha Swis 5,000 (Sh12,396,787).

Katika hukumu hiyo iliyokuwa na kurasa 29 imeeleza kuwa ushahidi uliotolewa na Yanga juu ya mkataba mpya uliotolewa na klabu hiyo ulikuwa na makosa mengi na kushindwa kuwa na ushahidi wa kutosha kama ulisainiwa na Morrison.

Akizungumza na Championi Jumatano, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa, katika hukumu kuna maamuzi mawili kushinda na kushindwa, hivyo Wanayanga wasahau hayo na badala yake kurejesha nguvu katika Ligi Kuu Bara.

“Wao (Simba) wametushinda CAS, basi na sisi Yanga tunatakiwa kuwashinda uwanjani kwa matokeo mazuri tutakapokutana nao Desemba 11, mwaka huu katika mchezo wa ligi.

“Tulikuwa tuna matarajio makubwa ya kushinda kesi hii CAS, hiyo ndiyo sababu ya kutumia gharama kubwa ya kukata rufaa CAS baada ya maamuzi ya utata TFF.

“Hivyo Wanayanga tunatakiwa kuungana kwa pamoja katika kuisapoti timu yetu katika michezo ya ligi na kikubwa kuchukua ubingwa huo katika msimu huu na Kombe la FA,” alisema Mwakalebela.

ALICHOSEMA EDO KUMWEMBE KUHUSU UWEZO WA ‘FEI TOTO’..ADAI NI YULE YULE TU..HANA JIPYA… AMRI KIEMBA : KUNA TATIZO AZAM FC..AFUNGUKA SUALA LA WACHEZAJI KUSIMAMISHWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply