News

‘FEI TOTO’ ASHINDWA KUJIZUIA YANGA…AAMUA KUFUNGA MAPYA KUHUSU UBINGWA KUTUA JANGWANI…

admin November 25, 2021 5:30 am


KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameweka wazi kuwa wao kama wachezaji wanaendelea kujipanga kuhakikisha wanapata alama tatu kwenye michezo yao inayofuata kwani msimu huu wana jambo lao hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi.

Yanga hadi sasa inaongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 16 katika michezo yote sita iliyocheza hadi sasa huku ikifuatiwa na Simba wenye pointi 14.

Akizungumza na Championi Jumatano, Feisal alisema kuwa kama safari ndio kwanza imeanza ya kusaka ubingwa, hivyo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata alama tatu kwenye mechi zao zinazofuata.

“Tunamshukuru Mungu hadi hapa tulipofikia tunaongoza ligi lakini hiyo pekee haitoshi kutufanya turidhike, hivyo tunaendelea kupambania malengo ya timu kwa sababu sisi wachezaji ndio tuna dhamana kubwa ya kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri kwa kupambana uwanjani.

“Kwa hiyo kitu pekee ninachoweza kuwaambia mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi kwani tumejipanga vizuri sana msimu huu tuna jambo letu kubwa ambalo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu litatimia,” alisema mchezaji huyo.

KISA AUCHO…YANGA YAWAITA SIMBA MEZANI..MWENYEWE AFICHUA MKATABA WAKE..CHAMA APELEKWA YANGA… KUELKEA MECHI YA JUMAPILI..WAZAMBIA WAINGIWA NA ‘MAWENGE’ DHIDI YA SIMBA MPYA YA PABLO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply