news

ALICHOKISEA AUCHO KUHUSU ISHU YAKE YA KUSEPA YANGA…ADAI YEYE NI MCHEZAJI…

admin November 26, 2021 12:14 pm


Kiungo kutoka nchini Uganda na klabu ya Young Africans Khalid Aucho amekanusha taarifa zinazomuandama kwa sasa, zikidai yupo njiani kuachama na klabu hiyo.

Aucho ameonekana kuwa nguzo imara katika nafasi ya kiungo kwenye kikosi cha Young Africans tangu alipotua klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo ambaye pia ni Nahodha Msaidizi wa kikosi cha Uganda amesema taarfa za kuhusishwa na mpango wa kuachana na Young Africans wakati wa dirisha dogo amezisikia, na amezipuuza kutokana na kuamini hana pakwenda zaidi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

“Sina mpango wa kwenda kokote, mimi bado ni mchezaji wa Yanga,” amesema Aucho kwa kifupi.

Khalid Aucho alisajiliwa Young Africans akitokea nchini Misri alipokua akiitumikia klabu ya El Makkasa ambayo alimsajili kuanzia mwaka 2019–2021.

KISA PENATI YA UTATA YA YANGA DHIDI YA NAMUNGO …BODI YA LIGI WAIBUKA NA HILI JIPYA… ALICHOKISEMA ‘BATGOL’ KUHUSU NANI MKALI ZAIDI  KATI YA KAGERE NA MUGALU….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply