Home BIashara United BAADA YA KUTOLEWA RASMI KWENYE KOMBE LA SHIRIKISHO..UONGOZI BIASHARA UTD WATOA YA...

BAADA YA KUTOLEWA RASMI KWENYE KOMBE LA SHIRIKISHO..UONGOZI BIASHARA UTD WATOA YA MOYONI…


SIKU chache baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Biashara United umesema ukata umekatisha safari ya mafanikio kwenye mashindano hayo huku wakibainisha kuwa bado wana nafasi ya kushiriki msimu ujao.

Akizungumza hivi karibuni, katibu mkuu wa klabu hiyo Haji Mtete alisema walikuwa wamejiandaa kisaikolojia kwa lolote watakalolipata, hivyo haikuwa sapraizi kwao na baada ya kuondolewa kwenye mashindano hayo nguvu zao wanahamishia Ligi Kuu na wana imani watapata nafasi kama hiyo.

Alisema walikuwa na kazi kubwa kuwatuliza wachezaji ambao waliamini mashindano hayo ni moja ya njia yao kujipatia mafanikio, lakini haijawa hivyo kutokana na ukata, hivyo kujikuta wanashindwa kukamilisha walichokuwa wamekipanga.

“Kwa upande wetu tulikuwa tumejiandaa kwa lolote, lakini kwa wachezaji tuliwahakikishia nafasi bado ipo ili waendelee kufanya vizuri kwenye ligi tukiwaambia kuwa ni moja ya maandalizi lakini imekuwa tofauti,” alisema nakuongeza kuwa.

Mtete aliongeza kuwa pamoja na kupata mechi mbili wamejifunza namna ya kujiandaa kwenye ushiriki wa mashindano ya kimataifa..

SOMA NA HII  KIPIGO KUTOKA MISRI JANA CHAMFANYA SAMATTA KUJA NA KAULI HII YA KISHUJAA...