Home news HUU HAPA MSIMAMO WA SIMBA KUHUSU ‘KUCHEZA MECHI NNJE YA UWANJA’…MATOKEO YATAJWA…

HUU HAPA MSIMAMO WA SIMBA KUHUSU ‘KUCHEZA MECHI NNJE YA UWANJA’…MATOKEO YATAJWA…


Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amevunja ukimya na kudai klabu yao haifanyi mipango ya nje ya uwanja ili kupata matokeo.

Mangungu ametoa kauli hiyo kwenye mkutano mkuu wa Simba unaoendelea Dar es Salaam.

Mangungu ameanza kwa kufichua kuwa mwaka huu ulikuwa mgumu kwa klabu yao hasa baada ya kuwapoteza watu mahiri ndani ya klabu hiyo.

Amesema kingine ni kuanza ligi vibaya msimu uliopita.

“Msimu huu tumeanza vizuri niweke wazi hili, kuna maneno maneno lakini Simba hatufanyi mipango nje ya uwanja, tunacheza uwanjani na kupata matokeo,” amesema Mangungu huku akitania kuwa kuna timu hadi penati inapigwa na watu wanane.

Mangungu pia amezungumnzia katiba ya klabu na kubainisha aina za wanachama ambao wapo waliokuwa na kadi za zamani na mpaka sasa hawajapata kadi mpya.

“Pia wanachama wenye kadi mpya lakini hawajaingizwa kwenye kumbukumbu za klabu na wale ambao wamelipia kadi zao na hawajapata, hilo tunalishughulikia.

Amesema kwenye matawi pia wana mkakati kila mkoa uwe na tawi la klabu hiyo linaloeleweka.

SOMA NA HII  BAADA YA 'KUICHINJA' SIMBA....KIIZA KWA KUJIAMINI AIBUKA NA HILI KUHUSU MABEKI WA SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here