Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA RUVU…..KAPOMBE AKIRI UBOVU SIMBA…ATOA AHADI MECHI YA...

KUELEKEA MECHI DHIDI YA RUVU…..KAPOMBE AKIRI UBOVU SIMBA…ATOA AHADI MECHI YA KESHO….


BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amekiri timu yao kuanza vibaya msimu huu na kuahidi mabadiliko makubwa kuanzia Ijumaa.

Simba inatarajia kushuka uwanjani CCM Kirumba Mwanza kumenyana na Ruvu Shooting ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 waliyoshinda katika uwanja huo msimu uliopita.

Kapombe amesema wameanza vibaya lakini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kusawazisha makosa yao kabla ya mchezo wao wa Ijumaa na kuwaahidi mashabiki wao furaha.

“Tupo imara ukiachana na majeruhi waliopo kikosini Simba ina kikosi kipana wachezaji tuliopo tunatosheleza kufanya vizuri kwenye michezo yote iliyo mbele yetu sio Ruvu Shooting pekee,” alisema na kuongeza kuwa.

“Simba tunakubaliana na kila hari lakini hatujawahi kukata tamaa kwa kuamini kuwa hatuwezi malengo yetu ni kutetea ubingwa tumejiandaa kwaajili ya ushindani kila mechi kwetu ni fainali,” alisema.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YOTE YANAYOTOKEA ...HUYU HAPA MCHEZAJI WA SIMBA MPOLE ASIYEIMBWA NA MASHABIKI WA SOKA...