Home news HATIMAYE…, TANZANIA YAFANIKIWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA MWAKANI…

HATIMAYE…, TANZANIA YAFANIKIWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA MWAKANI…


Wakati timu ya Taifa , Taifa Stars iliposhindwa kutumia vyema mchezo wake dhidi ya Congo DRC wa kuwania kufuzu kombe la dunia mwakani nchini  Qatar, Timu ya Taifa ya Soka la watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ imejikatia tiketi ya kucheza kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Uturuki.

Warriors wametumia takribani dakika 50 kujihakikishia ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Cameroon katika robo fainali ya mashindano hayo katikauwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha mkuu wa Tembo Warriors, Salvatory Edward amemuanzisha langoni Ally Juma huku katika eneo la ulinzi ni Abdulkarim khalifani, Shadrak Emblo na Juma kidem eneo la kiungo ni Ramadhani Chomelo na Frank Ngailo huku mshambuliaji ni Alfani Kiyanga.

Dakika 25 za kipindi cha kwanza zimewatosha Tembo Warriors kumaliza mchezo baada ya kupata mabao 3 ya mapema huku mshambuliaji wao Alfan Kiyanga akifunga mabao mawili pamoja na Ramadhani Chomelo.

Kipindi cha pili Warriors walirudi kwa kasi  licha ya kuwa mbele kwa bao 3-0 lakini waliongeza mengine mawili yaliofungwa na Frank Ngailo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa jumla ya mabao 5-0.

Akizungumza  mshambuliaji wa Tembo warriors Alfan Kiyanga amesema kujituma pamoja na juhudi ndizo sababu zilizopelekwa wao kupata ushindi huo.

“Bado tunasafari kuelekea kutwaa ubingwa lakini kikubwa ni umoja pamoja ushirikiano tulionao wachezaji pamoja na benchi la ufundi hivyo tuna matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika michezo inayofuata” amesema Kiyanga.

Kwa upande wa kocha Salvatory Edward amesema kua kiwango kilichoonyeshwa na timu yake hii leo ni kutokana na utayari pamoja na kucheza kwa morali ya juu huku wakijua taifa linawatizama wao.

Mchezo huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri wa sanaa utamaduni na michezo Innocent Bashungwa.

SOMA NA HII  WAGHANA KUWAFUATA MASTAA WA YANGA